Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva taxi kizimbani kwa kushika nyeti za mteja

Taxi Derava Dereva taxi kizimbani kwa kushika nyeti za mteja

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja ambaye ni dereva taxi jijini Nairobi amefikishwa katika Mahakama ya Makadara kwa madai ya kushika nyeti za mteja aliyekuwa akimpeleka uwanja wa ndege bila idhini ya mteja huyo.

Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Julius Keti alimshika mwanamke huyo ambaye ni mwanadiplomasia kutokea taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati alipokuwa akimsafirisha kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA ili kusafriri kurejea nyumbani kwao DRC.

Katika tukio hilo ambalo linadaiwa kufanyika mnamo Mei 30, mwanadiplomasia huyo anasemekana kuchukizwa na kitendo hicho cha dereva wa teksi ambacho alichukua hatua ya kuripoti katika ubalozi wa Kenya nchini Congo, huku maelezo yake yakielezea zaidi kwamba dereva huyo hadi alimkalia mapajani mwake.

Maelezo zaidi yalisema kwamba dereva huyo wa teksi aliegesha gari kando ya barabara na kuanza kumgusa pasi na idhini yake.

Mwanamke huyo raia wa Congo alikuwa amekwenda nchini Kenya kuhudhuria mkutano katika shule ya masomo ya kifedha (Kenya School of Monetary Studies) kabla ya kufanyiwa vitendo hivyo vya udharirishaji.

Bwana Keti aliachiliwa kwa dhamana ya laki mbili huku kesi hiyo ikitarajiwa kuendelea tena mnamo Septemba Mosi katika mahakama hiyo ya Makadara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live