Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dennis Bett aliyepata alama ya chini KCPE aibuka mshindi katika mtihani wa KCSE

Cfc976a3c931bbb1 Dennis Bett aliyepata alama ya chini KCPE aibuka mshindi katika mtihani wa KCSE

Wed, 12 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Waziri wa Elimu George Magoha alimpongeza Dennis Bett kwa kufanya vema katika mtihani wa kitaifa wa KCSE

- Licha ya Bett kupata alama ya 190 kwenye mitihani wake wa KCPE, aliweza kuvunja rekodi kwa kupata gredi ya B- katika mtihani wa KCSE

- Bett alisema alitia bidii masomoni baada ya kugundua makosa na udhaifu wake

- Mwanafunzi huyo pia aliwashukuru walimu kwa mwelekezo na usaidizi waliompa hadi akafaulu katika mtihani wake

Wakati Dennis Bett alipokea matokeo yake ya mtihani wa darasa la nane, KCPE wengi walidhani kwamba huenda ndio mwisho wake wa masomo kwani alikuwa amepata alama ya 190 pekee.

Hata hivyo, Bett hakukata tamaa kwani alipojiunga na shule ya upili, alikaza kamba na nia yake kuu ilikuwa ni kuwaabisha wakosoaji wake.

Miaka minne baada ya kufanya mtihani wa KCPE, Bett ameibuka miongoni mwa wanafunzi bora zaidi nchini kwa kujizolea alama ya B-.

Bett alikuwa kwenye orodha ya Waziri Magoha ya wanafunzi waliofanya vema zaidi katika mtihani wa KCSE kuliko walivyofanya katika mtihani wa KCPE.

Akizungumza na vyombo vya habari, Bett alisema aligundua makosa yake na ndio sababu alitia bidii alipojiunga na shule ya upili.

" Nilijua kilichonifanya nisifuzu katika mtihani wa KCPE na nikatambua nilichohitaji ili nipite mtihani wangu wa KCSE, kila mara nilikuwa najadiliana na walimu kuhusu dhana ya kupita mtihani," Alisema Bett.

Walimu wake walisema kwamba Bett alikuwa mwanafunzi mwenye nidhamu na alianza kufanya vema masomoni pindi alipojiunga na kidato cha kwanza.

Mwalimu wake Mkuu wa shule ya Kimargis Stephen Kirui alisema alijaribu kila awezalo kumsaidia Bett baada ya kuelewa familia aliyotoka.

Waziri wa Elimu George Magoha ni miongoni mwa viongozi ambao wamempongeza Bett kwa matokeo bora.

Akihutubia taifa Waziri Magoha alikuwa na haya ya kusema," Wanafunzi hao walikuwa wamepata alama ya 200 katika mitihani yao ya darasa la nane na kwa sasa wanatarajiwa kujiunga na vyuo vikuu, wengi walisomea katika shule za kaunti na wamefanya vema zaidi,"

Mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala kutoka shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliibuka mshindi kwa kupa gredi ya A ikiwa na pointi 87.33.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke