Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Deni la Tsh 8000 lasababisha mwenye duka kumuua mteja wake

Crime Scene Decoration  Mw 133583 2 Deni la Tsh 8000 lasababisha mwenye duka kumuua mteja wake

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Polisi katika Kaunti ya Bomet walimtia mbaroni mwenye duka ambaye aliyemuua mteja wake kufuatia deni la KSh 400.

Evans Mutai, mmiliki wa duka, alimdunga kisu Festus Keter kifuani wakizozania deni la KSh 400 Mwili wa Keter uligunduliwa na jirani yake aliyewaarifu maafisa kwenye Kituo cha Polisi cha Chesoen Mutai atafikishwa mahakamani mnamo Jumatatu Oktoba 25, ambapo atashtakiwa kwa mauaji.

Jumamosi, Oktoba 23, kuliibuka tukio ambapo Evans Mutai, ambaye ni mmiliki wa duka katika eneo la Sibaiyan alimdunga kisu Festus Keter, mwenye umri wa miaka 35, kifuani. Licha ya kutekeleza mauaji hayo, Mutai aliendelea na biashara yake ya kuwauzia wateja wake kama kawaida, hata asipigwe na mshipa.

Kulingana na ripoti ya ofisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai, Keter na Mutai walitupiana cheche za maneno kufuatia deni la KSh 400, mwendazake alilodaiwa na mwenye duka. Hatimaye Mutai alimdunga kisu Keter kifuani kwenye upande wa kulia, huku akimuacha akiwa amefariki dunia nje ya duka lake.

Mwili wake uligunduliwa na jirani ambaye aliwaarifu maafisa wa polisi katika Kituo cha Polisi cha Chesoen. Maafisa hao walifululiza hadi kwenye eneo la tukio lenye umbali wa kilomita 10 na kuanzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo ndiposa wakamkamata mshukiwa.

Silaha iliyotumika katika mauaji hayo, kisu kilichokuwa na damu, kilipatikana na kuwekwa kama ushahidi. Mutai atafikishwa mahakamani Jumatatu Oktoba 25, ambako atashtakiwa kwa mauaji.

Mwili wa Keter ulisafirishwa hadi chumba cha maiti cha Hospitali ya Longisa huku upasuaji wa maiti ukisubiriwa kufanywa.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke