Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Deep State wanajua Rais wa tano wa Kenya kabla ya wapiga kura

Eb4986ac36d7589f Deep State wanajua Rais wa tano wa Kenya kabla ya wapiga kura

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Katibu mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini (COTU) Francis Atwoli amesema 'deep state' tayari wanajua ni nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Atwoli amesema kwamba ni vigumu sana kumshinda mwaniaji anayeungwa mkono na 'deep state' kwa sababu wana pesa chafu. Atwoli pia alikiri kwamba kuna baadhi ya mataifa ya ughaibuni yenye mamlaka ambayo huyashawishi matokeo ya uchaguzi wa Urais kwa manufaa yao wenyewe.

Katibu mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini (COTU) Francis Atwoli amedai kwamba "deep state" wanajua ni nani atakayekuwa rais wa tano wa Kenya.

Akizungumza kwenye mahojiano na runinga ya TV47, Atwoli alisema kwamba 'deep state' wanajua ni nani atakayekuwa rais hata kabla ya Wakenya kupiga kura. Atwoli aliongeza kusema kwamba hakuna anayeweza kumshinda mwaniaji urais anayeungwa mkono na 'deep state.'

"Huwa wanajua kuyapiga mahesabu yao vizuri. Wanajua ni nani atakayekuwa rais hata kabla wapiga kura kujua. Hatimaye, wamtafuta mapema ili wafanye mkutano naye, ndiposa wajipange sawasawa kisha wasonge mbele. Na hutaweza kumshinda mtu kama yule," Atwoli alisema.

Uwepo wa 'deep state' Suala la 'deep state' limeibua mjadala miongoni mwa wanasiasa. Kulingana na utafiti uliofanywa na TUKO.co.ke, mnamo Agosti 2020, Wakenya wengi walikiri kwamba wanaamini kuna uwepo wa 'deep state'.

Mnamo Septemba 2021, Gavana wa Nyandarua Francis Kimemia alikiri pana uwepo wa 'deep state' katika siasa za Kenya. Gavana huyo alisema 'deep state' wanaweza kushawishi ushindi wa mwaniaji wamtakaye kwenye uchaguzi, ingawa haimaniishi kwamba watamsaidia kuiba kura.

Naibu Rais William Ruto katika siku za hivi majuzi alidai kwamba 'deep state' walikuwa wanapanga kumuibia kura kwenye uchaguzi mkuu wa 2022, madai ambayo yalipuuziliwa mbali na wanasiasa wanaomuunga mkono kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke