Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa za kulevya zenye thamani ya Sh9m zanaswa JKIA ndani viti vya baiskeli

Dawa Za Kulevya Zenye Thamani Ya Sh9m Zanaswa JKIA Ndani Viti Vya Baiskeli Dawa za kulevya zenye thamani ya Sh9m zanaswa JKIA ndani viti vya baiskeli

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) imekamata zaidi ya kilo 1 ya dawa ya methamphetamine yenye thamani ya Shilingi milioni 9m.

Kulingana na DCI, dawa hizo zilizonaswa siku ya Jumanne zilikuwa zimefichwa ndani ya tandiko za baiskeli na zilikuwa zikielekea mjini Jakarta, Indonesia.

Walisema shehena hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Moroni, Comoro.

"Wapelelezi waliotumwa katika uwanja wa ndege kukabiliana na uhalifu wa uhamiaji na mizigo inayotiliwa shaka ilikuwa imekusanyika katika kibanda cha DHL kwa ajili ya zoezi la uhakiki, ambapo vifurushi vya rangi ya kahawia vilipatikana vimefichwa kwenye viti vya baiskeli kumi na moja," DCI ilisema.

Vipimo vilithibitisha kuwepo kwa dawa aina ya methamphetamine.

DCI ilisema operesheni za interpol zimeanzishwa kutafuta wahusika ili wakamatwe na kufunguliwa mashtaka.

Idara za salama nchini Kenya zimeimarisha juhudi za kukabiliana na mihadarati nchini, pamoja na kutumia himaya ya Kenya kama kiunganishi cha usafirishaji wa mihadarati hadi mataifa ya kigeni.

Chanzo: Radio Jambo