Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa yenye ladha ya strawbery kutumika kwa watoto wenye HIV Kenya

Dozi Mpya Mpya Dawa yenye radha ya strawbery kutumika kwa watoto wenye HIV Kenya

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imeleta dawa yenye radha ya tunda la Strawberry kutumika kwa watoto wanaoishi na Upungufu wa Kinga mwilini UKIMWI.

Matibabu ya watoto hao kwa sasa yataolewa kwa kupewa dozi hii mpya ya dolutegravir, inayotumika kupambana na virusi hivyo iliyoidhinishwa na Shirika la Afya duniani, ambayo kwa sasa imebadilishwa ili kuweza kufanya matibabu hayo kuwa rahisi na kwa gharama nafuu.

Dozi hii mpya inatumika kwa kuchanganywa kwenye maji au juisi jambo ambalo linafanya watoto wengi kufurahia kuinywa badala ya kumeza vidonge.

Kenya inaungana na Uganda kuwa moja kati mataifa sita barani Afrika yanayotoa dozi hii ya dolutegravir yenye miligramu 10 pekee.

Mataifa mengine barani humu yamechukua hadi dozi 100,000 za dawa hii inayotolewa na Wakala wa wa Afya Dunia, Unitaid, pamoja na clinton Health Access Initiative(CHAI).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live