Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido afikisha wafuasi milioni 20 Instagram, amwacha mbali Diamond

Davido Pic Data Davido afikisha wafuasi milioni 20 Instagram, amwacha mbali Diamond

Fri, 23 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii wa muziki kutoka pande za Nigeria, Davido amefanikiwa kufikisha wafuasi (followers) milioni 20 katika  mtandao wa kijamii wa Instagram. Kwa matokeo hayo Davido,  anaendelea kushika namba moja kama msanii wa muziki mwenye idadi kubwa ya wafuasi kwenye mtandao huo Barani Afrika.

Ikumbukwe hadi kufikia mwishoni mwa  mwaka 2015 mkali  wa Bongofleva, Diamond Platnumz ndiye alikuwa msanii mwenye wafuasi  wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Afrika akiwa nao milioni 1.5.

Hata hivyo kufikia Septemba 2016 akaondolewa kwenye nafasi hiyo na Davido ambaye kwa sasa kafikisha wafuasi hao milioni 20, huku Diamond amefikisha  milioni 12.2.

Ukiachana na Davido, wasanii wengine wenye wafuasi wengi Instagram Afrika ni Yemi Alade milioni 13.7, Tiwa Savege milioni 13.4, Diamond milioni 12.2 na Wizkid milioni 12.1.

Kwa muktadha huo, Diamond hakupitwa na Davido pekee, bali hata Yemi Alade na Tiwa Savege wote kutokea pande hizo za Afrika Magharibi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Worldometer nchi ya Nigeria ina kadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 210, huku Tanzania ikiwa na watu  milioni 59.7, hivyo hilo linaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wasanii wa nchi hiyo kuwa na wafuasi wengi zaidi ya wanaotoka hapa nchini. Hata hivyo mpaka sasa mchezaji soka kutoka  Cristiano Ronaldo kutoka Ureno, ndiye binadamu mwenye wafuasi wengi zaidi duniani kwenye mtandao wa Instagram wakiwa  milioni 279, akifuatiwa na mwimbaji wa Marekani,  Selena Gomez mwenye anayefuatiliwa na watu  milioni 222.

Imeandikwa na Peter Akaro

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz