Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari Nigeria ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Daktari Nigeria Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha Jela Daktari Nigeria ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama nchini Nigeria imemhukumu mkurugenzi wa matibabu kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mpwa wa mke wake.

Dkt Olufemi Olaleye alimdhulumu msichana huyo kingono kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi mkewe alipojua na kuwaarifu polisi, mwendesha mashtaka alisema.

Daktari huyo alikana mashtaka wakati wa kesi hiyo.

Lakini hakimu katika mahakama ya Lagos alisema alipata ushahidi dhidi ya daktari kuwa na hatia na akakataa ombi lake la kuhurumiwa.

Olaleye alifikishwa mahakamani Novemba mwaka jana akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji kati ya Desemba 2019 na Julai 2022, msichana huyo alipoenda kuishi na familia yao.

Wakati wa kesi hiyo, mke wa daktari huyo, Aderemi Olaleye, alisema aligundua unyanyasaji huo baada ya msichana huyo kumwambia shangazi yake na dereva wa familia hiyo.Msichana huyo, ambaye sasa ana umri wa miaka 18, alisema daktari huyo amekuwa akilala naye na alitishia kumuua iwapo atamwambia mtu yeyote, mke wa daktari huyo alisema.

Pia alishtakiwa kwa kumlazimisha kutazama ponografia.

Mashahidi sita - msichana, mke wa mshtakiwa, daktari, mtaalamu wa malezi ya watoto na maafisa wawili wa polisi waliohusika katika uchunguzi - walitoa ushahidi katika kesi hiyo.

Daktari huyo pia alitoa ushahidi katika utetezi wake pamoja na daktari wake wa uchunguzi ambaye alikosea ushahidi wa matibabu uliotolewa na upande wa mashtaka.

Lakini wakati akitoa hukumu siku ya Jumanne, Hakimu Rahman Oshodi alisema ushahidi uliowasilishwa mbele ya mahakama "unamhusisha sana" mshtakiwa.

Jaji Oshodi alielezea mkurugenzi wa matibabu wa Optimal Cancer Care Foundation kama mkosaji "hatari" ambaye hakuonyesha dalili yoyote ya kujuta.

Kulingana na hakimu, maungamo ya awali ya Olaleye kwa polisi yalithibitisha kwamba alitenda makosa hayo.

Hakimu alikataa hoja za jopo la wanasheria wa daktari huyo kuwa msichana huyo alifunzwa na mke wa mshtakiwa kusema uwongo dhidi yake ikiwa ni mpango wa kuchukua mali yake.

"Kwa hivyo, nampata mshtakiwa na hatia kama alivyoshtakiwa," hakimu aliamua.

“Shitaka hili lina adhabu ya lazima ya kifungo cha maisha jela,” alisema.

Katika ombi lake la kuhurumiwa, wakili wa daktari huyo, Adebisi Oridate, aliomba serikali kutambua huduma za Olaleye kama daktari wa saratani na kwamba alikuwa mkosaji wa mara ya kwanza.

Lakini hakimu alitupilia mbali ombi hilo na kusema kwamba Olaleye lazima azuiliwe katika gereza hilo kwa muda mrefu kama dhibitisho kwamba mfumo wa haki wa Nigeria ulipuuza unyanyasaji wa kingono.

Pia aliamuru jina la daktari kuongezwa kwenye sajili ya wahalifu wa ngono ya Jimbo la Lagos.

Haijabainika iwapo daktari atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Chanzo: Bbc