Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari Kenya: Nilitibu watoto waliopigwa mabomu ya kutoa machozi bure

Daktari Kenya: Nilitibu Watoto Waliopigwa Mabomu Ya Kutoa Machozi Bure Daktari Kenya: Nilitibu watoto waliopigwa mabomu ya kutoa machozi bure

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Daktari wa Kenya ameambia BBC kwamba hospitali yake imewatibu watoto 53 bila malipo baada ya gesi ya kutoa machozi kurushwa darasani mwao na polisi wakati wa maandamano siku ya Jumatano.

"Kama mzazi, niliitikia kwa matumaini na kwa hofu, jambo ambalo lilinilazimu kuchukua hatua bila kuomba pesa," Dkt Aron Shikuku, kutoka hospitali ya kibinafsi ya Eagle Nursing Home katika mji mkuu, Nairobi, aliambia kipindi cha Newsday cha BBC.

Huduma ya afya nchini Kenya inaweza kuwa ya gharama kubwa huku asilimia 19 pekee ya watu wakipata aina yoyote ya bima ya matibabu - kulingana na takwimu za hivi punde za 2018.

Hospitali za umma nchini kwa kawaida hazina wahudumu wa kutosha na hazina vifaa vya kutosha huku gharama ya kupata matibabu katika hospitali ya kibinafsi mara nyingi inaweza kusababisha kulemaza kwa shughuli kutokana na deni la matibabu.

Dk Shikuku alisema watoto hao waliruhusiwa Kwenda nyumbani baada ya kutibiwa kwa mshtuko na matatizo ya kupumua kutokana na gesi ya kutoa machozi.

Alisema walikuwa wakifuatiliwa walipokuwa wakitulia katika shule yao, iliyoko Kangemi, eneo la makazi duni kaskazini-magharibi mwa jiji.

Kulikuwa na maandamano kote nchini yaliyoitishwa na upinzani juu ya kupanda kwa gharama ya maisha, lakini yaligeuka kuwa mauti.

Chanzo: Bbc