Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dahabu ya mabilioni ya dola husafirishwa kwa magendo kutoka Afrika-Ripoti

Dahabu Ya Mabilioni Ya Dola Husafirishwa Kwa Magendo Kutoka Afrika Ripoti Dahabu ya mabilioni ya dola husafirishwa kwa magendo kutoka Afrika-Ripoti

Thu, 30 May 2024 Chanzo: Bbc

Ripoti mpya inasema kuwa dhahabu ya thamani ya mabilioni ya dola inasafirishwa kimagendo kutoka Afrika kila mwaka.

Uchunguzi wa shirika la Swissaid umegundua kuwa nyingi ya dhahabu hiyo huishia kati Umoja wa Falme za kiarabu.

Swissaid imesema Umoja huo wa Falme za Kiarabu ndio kituo kikuu cha dhahabu hiyo kutoka Afrika ambako mji wa Dubai unatambulika kwa kuwa na soko kubwa la dhahabu,kisha badaye husafirishwa hadi nchi za Ulaya kama Uswisi,India na nyingine huishia Marekani.

Ripoti hiyo inasema Mali, Zimbabwe na Ivory Coast zinazalisha kiasi kikubwa zaidi cha dhahabu ambayo haisajiliwi rasmi.

Inakadiriwa kuwa karibu asilimia arobaini ya dhahabu ya Afrika husafirishwa nje ya bara hilo kimagendo na kiwango kimeongezeka mara mbili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Tani kati ya mia tatu na mia nne za dhahabu za thamani ya hadi dola bilioni thelathini na tano zinazozalishwa katika migodi midogo hazijulikani zinakoishia kila mwaka.

Shirika hilo la Swissaid linasema madini hayo yenye thamani kubwa ni chanzo cha vipato kwa wachimba madini,upatikanaji wa kodi kwa serikali nyingi za Afrika,lakini pia huchangia katika kufadhili makundi ya waasi na kuchangia katika vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na uchafuzi wa mazingira.

Ripoti hiyo inaangazia kipindi cha kati ya mwaka 2012 na 2022 na inajikita katika data zilizokusanywa kutoka nchi 54.

Chanzo: Bbc