Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yawakataa wanajeshi Rwanda

Rwanda Congo Askari DRC yawakataa wanajeshi Rwanda

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeafiki askari wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki watumwe mashariki mwa nchi hiyo kukabiliana na waasi kwa sharti kuwa wanajeshi wa Rwanda wasiwe katika kikosi hicho.

Msemaji wa Serikali ya Kinshasa, Patrick Muyaya amesema DRC katu haitaafiki wanajeshi wa Rwanda kujumuishwa kwenye kikao hicho.

Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao siku chache zilizopita waliuteka mji wa Bunagana. Rwanda imekanusha vikali madai hayo na yenyewe imeituhumu DRC kuwa inawaunga mkono waasi walio dhidi ya serikali ya Kigali.

DRC imetangaza msimamo huo kuelekea kikao cha wakuu wa majeshi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki watakutana jijini Nairobi, kuamua kutumwa kwa kikosi hicho cha pamoja, katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri.

Aidha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenyatta amewataka viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kufika Nairobi leo kujadili mpango wa kutuma askari wa kieneo katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kukabiliana na waasi. Rais Kenyatta ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi hivi karibuni ameituhumu Rwanda kwa kutaka kupora ardhi yake nchi yake ,"yenye utajiri wa dhahabu,

kobalti na madini mengine, kwa ajili ya kujinufaisha."

"Hali ya usalama mashariki mwa nchi inaendelea kuzorota, na kimsingi kwa sababu Rwanda inataka kumiliki ardhi yetu, yenye utajiri wa dhahabu, koltani na kobalti, kwa ajili ya unyonyaji na faida yao," rais wa DRC amesema. "Hivi ni vita vya kiuchumi kwa ajili ya kupigania rasilimali, na magenge ya kigaidi ya Rwanda yanaongoza vita hivi."

Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kwa kifupi kama MONUSCO, tayari kipo nchini DRC lakini hakijaweza kuwazuia waasi na makundi ya wabeba silaha kutekeleza jinai mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Tshisekedi wa DRC alitoa wito kwa viongozi wa kimataifa kuishinikiza Rwanda hasa wakati wikii ambapo Rwanda ni mwenyeji wa mkutano wa Jumuiya ya Madola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live