Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yawaagiza maafisa wa Rwanda kikosi cha kanda ya EAC kuondoka nchini humo

DRC Yawaagiza Maafisa Wa Rwanda Kikosi Cha Kanda Ya EAC Kuondoka Nchini Humo DRC yawaagiza maafisa wa Rwanda kikosi cha kanda ya EAC kuondoka nchini humo

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Jeshi la DRC limesema "kwa sababu za kiusalama" limewaamuru kuondoka nchini humo maafisa wa Rwanda waliokuwa wanachama wa Kamandi ya Vikosi vya Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoko Goma, DRC.

Katika taarifa, msemaji wa jeshi Jenerali Maj Sylvain Ekenge alisema maafisa hao "tayari wameondoka katika ardhi ya Congo".

Inaongeza kuwa hii iliifanya Rwanda "kuwaita maofisa wake wote" ambao walikuwa wanachama wa mifumo ya kikanda iliyoko DRC.

"Si Rwanda ambayo imewaita maafisa hao. Ni DRC ambayo imewafukuza,” msemaji wa jeshi la Rwanda Brig. Jenerali Ronald Rwivanga aliambia BBC siku ya Jumanne.

DRC imewakataa wanajeshi wa Rwanda kuwa sehemu ya wanajeshi wa kanda linaloongozwa na Kenya waliotumwa mwaka jana katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC.

Lakini maafisa wachache wa Rwanda walikuwa sehemu ya kamandi ya kikosi hiki, pamoja na Utaratibu Ulioboreshwa wa Uthibitishaji wa Pamoja wa Mkutano wa Kimataifa wa Eneo la Maziwa Makuu (ICGLR).

Mvutano kati ya Kigali na Kinshasa umezidi kuwa mbaya wiki iliyopita wakati jeshi la Rwanda lilipopiga kombora ndege ya kivita ya Congo karibu na uwanja wa ndege wa Goma. Utaratibu wa uthibitishaji wa kikanda umewekwa ili kuchunguza tukio hilo.

Kinshasa inaishutumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, jambo ambalo Kigali limekuwa likikanusha.

Chanzo: Bbc