Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yatia saini makubaliano na muwekezaji wa Israel kurejesha mali zake

Drc Ventura DRC yatia saini makubaliano na muwekezaji wa Israel kurejesha mali zake

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo imetia saini "makubaliano ya kirafiki na Kundi la Ventura la mfanyabiashara wa Israel Dan Gertler" ili kumaliza mzozo wa kisheria kati yao na kuruhusu nchi hiyo kurejesha baadhi ya mali, serikali imetangaza.

“Kwa mujibu wa maagizo ya Rais wa Jamhuri, mkataba huu unaruhusu nchi ya Congo kurejesha madini na mafuta yenye mgogoro wa kundi la Ventura. Hili ni la kwanza la kihistoria kwa nchi hiyo, ambayo kwa hivyo inarudisha mali ambayo uuzaji wake ulitiliwa shaka,” huduma ya mawasiliano ya rais wa DRC ilisema Ijumaa.

"Kwa hivyo serikali ya Kongo itathamini mali hizi kwa manufaa ya Umma"

Mkataba na Ventura ulitiwa saini siku ya Alhamisi.

Kwa mujibu wa serikali, vitalu na mali zitakazorudishwa zina thamani ya zaidi ya dola bilioni 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live