Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yatangaza siku tatu za maombolezo kwa waathiriwa wa mauaji

DRC Yatangaza Siku Tatu Za Maombolezo Kwa Waathiriwa Wa Mauaji DRC yatangaza siku tatu za maombolezo kwa waathiriwa wa mauaji

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa waathiriwa wa mauaji yanayodaiwa kutokea mashariki mwa nchi hiyo.

Ni hatua isiyo ya kawaida sana baada ya miaka mingi ya machafuko katika eneo hilo, lakini Felix Tshisekedi alisema zaidi ya watu mia moja wameuawa katika kijiji cha Kishishe.

Amewalaumu waasi wa M23 kwa mauaji hayo, jambo ambalo wanalikanusha. Kumekuwa na milipuko ya ghasia kali tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda kukubaliana kusitisha mapigano wiki iliyopita.

Kongo, Marekani na Umoja wa Mataifa zimeishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la M23 lakini Kigali inakanusha madai hayo.

Kuna juhudi za kuleta amani mashariki mwa nchi hiyo zinaozoendelea nchini Kenya na tayari mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki yametuma vikosi ili kupambana na makundi yenye silaha nchini DRC.

Chanzo: Bbc