Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yaripoti zaidi ya vifo 120 vya mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo

Menigist Cong DRC yaripoti vifo 129+ vya Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya afya Nchini Congo, imetangaza vifo 129 kufduatia kuibuka kwa uogonjwa wa mlipuko wa uti wa mgongo 'Meningitis' unaosambaa kwa kasi sawa na ungonjwa wa UVIKO -19.

Wizara hiyo imeeleza kuwa ugonjwa huo unaathiri sana uti wa mgongo pamoja na ubongo, na unambukizwa kwa njia za upumuaji, kama vile kugusa makoozi au ute wa mtu mwenye maambukizi.

Ugonjwa huo hauna tiba ya moja kwa moja na mara nyingi huathiri ubongo na kupelekea mtu kuwa kiziwi, na kwa watoto wadogo huenda kuathiri moja kwa moja afya ya ubongo. wataalamu wanaeleza kuwa ugonjwa huu unaingia kwenye kundi la magonjwa ya mlipuko.

Wametaja dalili kuu za ugonjwa huo kuwa ni maumivu makali ya kichwa, homa pamoja na uchovu, huku wakibainisha kuwa ni ngumu kwa mtu kutambua kwa haraka kama ana dalili za ugonjwa huo kwani zinafanana na dalili za magonjwa mengine yaliyo na yasiyo ya mlipuko.

Hata hivyo wizara hiyo imesema kuwa tayari wameshafanya mchakato wa kusambaza timu ya madakati kwa kushirikiana na Shirika la Afya dunia la WWHO ili kuweza kupambana na kasi ya mlipuko huo walio utaja kuwa sawa na UVIKO-19 katika usambaaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live