Thu, 4 Feb 2021
Chanzo: habarileo.co.tz
Wabunge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamemchagua Christophe Mboso N'Kodia Pwanga (78) kuwa Spika mpya wa Bunge, nchini humo.
Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii (BBC),wadhifa huo ameupata baada ya kupata kura nyingi kutoka kwa wabunge katika uchaguzi uliofanyika jana.
Pwanga amechukua nafasi ya spika wa zamani, Jeanine Mabunda aliyeondolewa, mapema mwezi Desemba kwa madai ya ubadhilifu wa fedha za Bunge.
Aidha, taarifa hiyo imesema spika huyo mpya atajiunga na wabunge 391 kuunda serikali mpya ya rais wa sasa wa DRC, Felix Tshisekedi.
Chanzo: habarileo.co.tz