Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yakumbwa na wimbi la tatu la corona

003931b39f12cc32ee556de4e767fe48.jpeg DRC yakumbwa na wimbi la tatu la corona

Sat, 5 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jean-Jacques Mbungani amesema nchi hiyo inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Katika taarifa yake, Waziri Mbungani alisema jiji la Kinshasa limeathiriwa zaidi na maambukizi ya virusi hivyo na kwamba ndani ya wiki nne zilipotika kumekuwa na ongezeko kubwa la waathirika wa ugonjwa huo sambamba na idadi ya vifo kuongezeka.

Alisema kirusi kipya aina ya Delta kutoka India na kingine cha Beta kutoka Afrika Kusini ndivyo vinavyosumbua kwa sasa nchini humo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema kuanzia Mei mwaka huu, virusi aina ya SARS-Cov-2 vimekuwa vikishambulia kwa wingi katika jiji hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO barani Afrika, Dk Matshidiso Moeti, ameonya kuwa DRC pamoja na mataifa mengine ya Afrika yapo katika hatari ya kuathiriwa na mlipuko wa tatu.

WHO ilisema kuwa upatikanaji wa chanjo barani Afrika kwa haraka ndio suluhu ya kuzuia ongezeko la maambukizi ya vizuri hivyo visizidi kuenea kwa kasi na kuleta athari.

Chanzo: www.habarileo.co.tz