Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yakomaa wanajeshi EAC kuondoka nchini

UN MAUJAI DRCCCCC DRC yakomaa wanajeshi EAC kuondoka nchini

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inasema vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki vimeshindwa kurejesha amani mashariki mwa taifa hilo na kutoa wito kwa jeshi hilo kuondoka kufikia mwezi Desemba.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa serikali ya Kongo, Patrick Muyaya, ni dhahiri kuwa vikosi hivyo vimeshindwa kutatua changamoto iliyopo ya kiusalama.

Waasi wa M23 wameonekana kukaidi makubaliano yaliotiwa saini mwaka jana jijini Luanda Angola, yakuwataka kuondoka katika sehemu wanazokalia.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, wanajeshi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Uganda, Burundi, Sudan Kusini na Kenya, walitumwa katika eneo la Kivu Kaskazini kurejesha utulivu na amani. Makundi ya waasi yamekuwa yakiripotiwa kuwashambulia raia licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa EAC Makundi ya waasi yamekuwa yakiripotiwa kuwashambulia raia licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa EAC © Alexis Huguet / AFP

Eneo la Mashariki ya Kongo, kwa muda sasa, limekuwa likikabiliwa na utovu wa usalama, makundi ya watu wenye silaha yakiwa changamoto kwa raia wa sehemu hiyo licha ya kuwepo wa vikosi vya walinda usalama wa UN tangu mwaka wa 1999.

Mwaka uliopita, viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliwaagiza waasi wa M23 kuachana na mapigano na kuondoka katika maeneo wanayokalia. Waasi wa M23 wamekataa kuondoka katika maeneo wanayokalia licha ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa nchi za EAC Waasi wa M23 wamekataa kuondoka katika maeneo wanayokalia licha ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa nchi za EAC © EAC

Licha ya agizo hilo, waasi hao mwezi Aprili, walikataa kuondoka baada ya rais Félix Tshisekedi kuwatenga kwenye mazungumzo.

Rais Tshisekedi, ambaye anawania tena katika uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba, amewataka wanajeshi wa UN kuondoka mwaka huu nchini mwake badala ya mwaka ujao kama ilivyopângwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live