Mjumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Umoja wa Mataifa , Georges Nzongola-Ntalaja, ameishutumu Rwanda, bila kuwa na ushahidi kwamba, inachukua sokwe kutoka misitu ya Congo na kuwapeleka Rwanda.
Bwa Nzongola-Ntajala alisema hayo wakati wa kikao cha dharura cha 11 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kujadili na kupigia kura azimio la Urusi kunyakua mikoa minne ya Ukraine.
Aliishutumu Rwanda kwa kuikalia Kongo "mwaka 1998 hadi 2003" kupora dhahabu na coltan "na rasilimali nyingine nyingi".
"Wanachukua hata sokwe na sokwe kutoka misitu ya Kongo wakiwapeleka Rwanda, yote haya yanajulikana," Bw Nzongola-Ntajala aliongeza.
Rwanda, Uganda, na DR Congo zinashiriki volkano kubwa kati ya mipaka yao ambayo ni nyumbani kwa sokwe wa milimani adimu.
Mjumbe wa Rwanda Robert Kayinamura alionekana kubeza kauli ya Bw Nzongola-Ntajala.
"Madai haya ... kila wakati maji yakikosekana- ni Rwanda, umeme ukipotea - ni Rwanda, ikiwa hakuna barabara ni Rwanda ... tunahitaji kuondokana mitazamo kama hii," Bw Kayinamura alisema.