Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema ina "ushahidi mkubwa" unaoonyesha hatua dhidi kuvuruga hali ya usalama wa taifa hilo.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Rais wa taifa hilo imebainisha hayo siku ya jumenne.
Katika taarifa yake iliyosomwa kwanjia ya televisheni taifa, Msemaji wa Rais Kasongo Mwema alisema jaribio la namna hiyo la "kuvuruga taasisi za kidemokrasia" halitavumiliwa.
Hatua hiyo inafuatia mara baada ya kukamatwa kwa mshauri maalum wa usalama wa Rais FĂ©lix Tshisekedi bwana Francois Beya siku ya Jumamosi.
Tukio hilo lilitokea wakati Rais wa taifa hilo alipokuwa akihudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Kukamatwa huko kulizua maandamano, huku wanachama wa chama cha Rais wakiingia mitaani kupingwa kukamatwa kwake.
Msemaji wa Rais alisema uchunguzi unaendelea na hali imedhibitiwa.
Kimya kutoka kwa serikali na Afisi ya Rais tangu kisa hicho cha Jumamosi kimechochea tetesi za ukosefu wa utulivu na amani nchini humo.
Si Bwana Beya wala mawakili wake ambao wametoa taarifa yoyote kwa umma kuhusiana na kukamatwa kwake.