Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yaanza kuandikisha wapigakura

Kuraaa.png DRC yaanza kuandikisha wapigakura

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeanza usajili wa wapiga kura ili kujiandaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika Desemba 2023.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Aljazeera, Rais Felix Tshisekedi anatarajiwa kugombea tena urais baada ya muhula wa kwanza.

Takriban watu milioni 50 katika majimbo 26 ya taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati wanatarajiwa kujiandikisha kupiga kura katika muda wa miezi mitatu ijayo ambapo uandikishaji huo umeanza Desemba 23, 2022.

“Hakuna mashine, walipaswa kuahirisha badala ya kupanga tarehe na kisha kutofanya lolote watu wanapofika,” alisema mwanafunzi wa Kitiba Mike Tshamala, akisubiri pamoja na wengine katika kituo cha kujiandikisha katikati mwa Kinshasa.

Tume ya Uchaguzi (CENI) ilizindua mfumo mpya wa usajili wa awali wa simu za rununu ili kuharakisha mchakato na kuzuia misururu mirefu iliyojitokeza wakati wa uchaguzi uliopita.

Lakini vituo vingi vya usajili katika mji mkuu, Kinshasa, vilishindwa kufunguliwa kama ilivyopangwa kutokana na ukosefu wa wafanyakazi.

Muangalizi wa uchaguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia Reuters ni vifaa 6,900 pekee kati ya zaidi ya 11,000 vinavyohitajika kwa awamu ya kwanza ya usajili viliwasili mwanzoni mwa wiki iliyopita.

"Ni kama gari, unaanza kwa gia ya kwanza, hauendi moja kwa moja kwenye gia ya tatu," Mwenyekiti wa CENI Denis Kadima alisema baada ya kujiandikisha mjini Kinshasa.

Tshisekedi, 59, pia alisajiliwa Jumamosi katika mji wa kaskazini magharibi wa Mbandaka, ambapo mlipuko wa Ebola ulitokea mapema mwaka huu.

Martin Fayulu, mshindi wa pili katika kura ya urais, tayari ametangaza nia yake ya kuwania tena.

Kiongozi wa upinzani Moise Katumbi ambaye ni gavana wa zamani mwenye nguvu wa jimbo la Katanga linalozalisha shaba, pia ametangaza kugombea nafasi ya urais.

Uchumi wa DRC umeathiriwa na janga la Uviko-19 na vita vya Ukraine tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019.

Ukosefu wa usalama umeongezeka mashariki mwa DRC tangu waasi wa M23, ambao mamlaka wanashutumu nchi jirani ya Rwanda kuwaunga mkono, kufanya mashambulizi makubwa mwezi Machi mwaka huu.

Rwanda inaendelea kukanusha kuhusika kuwaunga mkono M23, licha ya kauli tofauti kutoka kwa wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live