Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC yaanza kuachia huru wafungwa kupunguza msongamano

Wafungwa Drc Kinshasa.jpeg DRC yaanza kuachia huru wafungwa kupunguza msongamano

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafungwa wapatao 7,000 wataachiliwa huru kwa masharti kutoka kwenye jela kuu ya Makala iliyoko katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa katika jitihada za kupunguza msongamano wa wafungwa wanaoshikiliwa katika jela hiyo.

Makala, ndiyo jela kubwa zaidi nchini DRC, ambayo ilijengwa mwaka 1957 kwa ajili ya kupokea wafungwa 1,500, lakini hivi sasa inashikilia zaidi ya wafungwa 15,000, wakiwemo watoto na wanawake.

Hali ni mbaya sana katika gereza hilo huku wafungwa wakiwa wamejazana ndani ya seli, wakila vibaya na wengine kuugua maradhi yanayosabishwa na kunywa maji yasiyo salama na matatizo ya kupumua.

Siku ya Jumamosi, Waziri wa Sheria Constant Mutamba aliidhinisha kuachiliwa huru kundi la kwanza la wafungwa 421 na kutangaza kuwa wafungwa hao elfu saba watakuwa wakiachiliwa huru kwa idadi ya watu 400 kila wiki.

Constant Mutamba Mutamba aliendelea kueleza kwamba, juhudi zinaendelea kufanywa ili kupunguza msongamano katika magereza yote ya Kongo DR na kuongeza kuwa imeundwa tume maalumu kuchunguza kesi za wafungwa wanaostahili kuachiliwa kwa masharti.

Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameagiza kuachiliwa huru wafungwa ambao ni wagonjwa na watoto kutoka jela kuu ya Makala na amepiga marufuku kupokewa wafungwa wapya katika jela hiyo. Amesisitiza kuwa, lengo la hatua hiyo ni kupunguza idadi ya wafungwa katika jela hiyo kuu ya DRC hadi kufikia nusu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live