Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC na SADC kuanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa M23

Mapigano Makali Yanaendelea Vikosi Vya Serikali Na Waasi Wa M23 DRC na SADC kuanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa M23

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya Maendelezo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC dhidi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.

Maafisa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congona wale wa kikosi cha mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, wamefanya mkutano wa tahmini ya hali ya kiusalama jimboni Kivu ya Kaskazini.

Kufuatia mkutano huo, Luteni Jenerali Fall Sikabwe, Kaimu Mkuu wa jeshi la Kongo DR amesema kuwa, jeshi la FARDC na kikosi cha SADC maarufu SAMIDRC wataanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa M23.

Kwa upande wake, naibu kamanda wa kikosi cha SADC nchini Kongo , Jenerali Julius Gambos kutoka Tanzania amesema lengo la kikosi hicho ni kuunga mkono jeshi la Kongo kuyasaka makundi ya waasi huko kwenye majimbo ya mashariki. Waasi wa M23

Kikosi hicho cha SAMIDRC kinajumuisha wanajeshi kutoka Malawi, Afrika Kusini, na Tanzania. Kundi la kwanza la wanajeshi wa kikosi hicho kutoka Afrika Kusini liliwasili mjini Goma Desemba 15 mwaka jana.

Serikali ya Jamhurii ya Kidemokrasia ya Congo, ilialika kikosi hicho cha SADC baada ya kusema kuwa haijaridhika na wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao walitakiwa kupambana na waasi wa M23.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikimtuhumu jirani yake Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yamekanushwa na Kigali, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live