Mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na Rwanda, wamekubaliana kuharakisha juhudi za kupunguza mvutano na kutatua mzozo wao wa kisiasa.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wao nchini Angola, mawaziri hao walikubaliana kuendelea kuyapa kipaumbele mazungumzo kama njia ya kutatua mgogoro wa kisiasa kati ya mataifa hayo mawili na kuelezea ratiba ya kuharakisha mpango wa kupunguza mvutano huo uliotiwa saini mwezi Julai.
Marekani yaishauri Ukraine ‘kuomba poo’ vita na UrusiWatano wauawa jirani na kambi ya JeshiMpango huo wa kumaliza uhasama, ulifikiwa katika mkutano wa kilele uliosimamiwa na Angola kati ya Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Kongo Felix Tshisekedi, hatua ambayo inakuja baada ya DRC kufukuza Balozi wa Rwanda nchini kwake.
Uhusiano wa kikanda katika eneo la Afrika ya Kati umedorora katika miezi ya hivi karibuni, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi ambao wamesababisha maelfu ya watu kukimbia makaazi yao.