Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Zaidi ya watu laki 6 wamethiriwa na mafuriko katika jimbo la Équateur

Mvua Imesababisha Vifo Vya Watu 4 Huko DRC DRC: Zaidi ya watu laki 6 wamethiriwa na mafuriko katika jimbo la Équateur

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu laki 6, wanaripotiwa kuathiriwa na mafuriko makubwa ambayo yamekuwa yakishuhudiwa Katika jimbo la Équateur, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kutokana na mvua ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika eneo hilo, shirika la Caritas, linasema hadi kufikia sasa ni takirban watu laki sita na elfu 86 ambao wameathirika.

Mafuriko hayo aidha yamesababisha uharibifu wa nyumba na barabara, shirika hilo sasa likitoa wito wa misaada ya chakula, makazi na huduma za afya.

Kulingana na mwakilishi wa shirika hilo, Louis Iyeli, ameelezea hali kuwa mbaya, ambapo watu wamelazimika kuishi kwenye maeneo ambayo maji yameendelea kuongezeka kina kila siku.

Anasema mabali na makazi ya watu kuharibiwa, miundombinu ya shule, na makanisa na vimlevile vituo vya afya imeharibiwa, huku pia kukiwa na hofu ya kutokea milipuko ya magonjwa kutokana na mafuriko hayo, wito wa msaada ukitolewa kwa serikali kuweka mikakati ya kushughulikia suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live