Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Yaishutumu Rwanda, M23 kwa kuhatarisha usalama wa anga

DRC: Jeshi Larejesha Utulivu Katika Mji Mdogo Wa Sake Uliodhibitiwa Na M23 DRC: Yaishutumu Rwanda, M23 kwa kuhatarisha usalama wa anga

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kongo inaishutumu Rwanda kwa kufanya "mashambulizi ya kutisha" mashariki mwa DRC ili kudhoofisha usalama wa anga.

Kulingana na Kinshasa, uchunguzi wa kiufundi ulifichua wajibu wa jeshi la Rwanda na waasi wa M23 katika uhalifu huo. DRC imetangaza kuwa imewasilisha malalamiko yake kwa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga.

DRC inahusisha moja kwa moja Rwanda na M23, wanaoendesha harakati zao huko Kivu Kaskazini, katika shughuli za hatarisha usalama katika eneo la mashariki mwa Kongo.

DRC imesema wanafanya hivyo kwa kuingilia mfumo wa mawasiliano unaotumia teknolojia ya GPS. Katika taarifa yake iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumanne , serikali ya Kongo imesema ilifanya uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu kwenye mfumo wa mawasiliano ya kuongoza ndege unaotumia teknolojia ya GPS baada ya ripoti za kuwepo mparaganyiko.

Taarifa hiyo imesema uchunguzi wake umegundua vikosi vya jeshi la Rwanda ndiyo vimehusika kusababisha hitilafu hiyo kwa kuhujumu mfumo uliopo. Imesema vikosi hivyo vimekuwa vikituma mawimbi tofauti ya mawasiliano ya GPS kwa dhamira ya kuvuruga ule uliopo."Vitendo hivi vinahujumu usafiri wa anga" na "kuhatarisha misheni muhimu ya kibinadamu" kulingana na Kinshasa.

Anga iliyoathiriwa ingeanzia Goma hadi Beni, ikijumuisha Butembo, Kanyabayonga na Kibumba. Kwa mujibu wa Wizara ya Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Kongo, vitendo hivi "vinalinganishwa na matumizi ya silaha za vita dhidi ya walengwa wa kiraia" na vinaonyesha "imethibitishwa kuwa Rwanda inakiuka sheria za kimataifa na ulinzi wa maisha ya raia". DRC imewasiliana na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga ili kupata vikwazo dhidi ya Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live