Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Waziri Jean Pierre Bemba amefanya ziara mjini Goma

CAAD2CBB 60C1 4468 A9FA 48BEDA08623E.jpeg DRC: Waziri Jean Pierre Bemba amefanya ziara mjini Goma

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa ulinzi nchini DRC, Jean Pierre Bemba, aliwasili jijini GOMA hapo jana, ziara yake anayoifanya wakati huu vikosi vya serikali vikizidisha mashambulio dhidi ya waasi wa M23 waliokuwa wanadaiwa kuelekea kwenye mji huo.

Kwa mujibu wa waziri Bemba, alikuwa Goma kuwaona waliojeruhiwa kutokana na vita pamoja na kuzisaidia familia 12 zilizowapoteza wapendwa wao kuweza kuwazika waliofariki.

“Ni ujumbe wa faraja na kutoa msaada pia kwa rafiki zetu wanajeshi waliopo hapa wa SADC, makampuni binafsi ndugu zetu wazalendo,ambao nao wanapigana tunawapongeza kwa ulinzi wa eneo letu " alisema waziri Bemba.

Aidha kiongozi huyo alitoa wito kwa raia katika mkoa wa Kivu kaskazini kuwa watulivu wakati huu ambapo mkuu wa nchi anafuatilia kwa karibu hali kwenye eneo hilo.

Vilevile amewaeleza raia kuwa jeshi la nchi yake linafanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Goma, Sake na maeneo mengine yote yanalindwa pamoja na eneo lote na Masisi na Rutshuru ilikuona kuwa raia wanakombolewa kutoka kwa M23.

Pasi Mubalama anatoka katika shirika la kiraia la wanawake la Aidprofen.

“Ni sharti wapigane iliwawaondoe M23 kila mahali ambapo wanapopatikana kwa sababu sio Goma tu.” alieleza Pasi Mubalama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live