Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Watu wengi watoroka makazi yao kufuatia mapigano mapya

GOMA DRC.png DRC: Watu wengi watoroka makazi yao kufuatia mapigano mapya

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wengi wametoroka makaazi yao kutoka maeneo ya Rutshuru na Masisi katika mkoa wa Kivu Kazkazini na kukimbilia katika eneo la Kanyabayonga katika vilaya ya vijijini ya Lucro kufuatia kuzuka kwa mapigano maya kati ya makundi yenye silaha yanayounga mkono serikali na kundi na waasi wa M2, wanaodaiwa kuwa wanasaidiwa na Rwanda.

Kutoka kwa mazingira yao ya asili hadi Kanyabayonga watu hawa waliofurushwa makwao wanapitia masaibu, kulingana na Radio OKAPI inayorusha matangazo yake DRC.

Watu hawa wanakimbia maeneo ya Nyanzale, Kirima, Kitchanga, Kachalira na Kibirizi katika maeneo ya Rutshuru na Masisi.

Wengi wao, wakiwemo watoto, husafiri kati ya kilomita 25 na 75 kwa miguu kabla ya kufika katika wilaya ya vijijini ya Kanyabayonga katika eneo la Lubero.

Kulingana na Zacharie Mumbere Lubuto, makamu wa rais wa kamati ya eneo la watu hawa waliohamishwa, baadhi ya wanawake waliohamishwa walibakwa wakiwa njiani kutoroka:

“Kwa wanawake waliokimbia makazi yao kutoka Kibirizi, Kashalira, Kirima, Nyanzale, Kichanga, wengi walibakwa wakati wa kukimbia kwao. Wnawake wanne walibaikwa walipokuwa njiani kuelekea Kyasenda ndipo wanawake wanane walibakwa.”

Katika eneo la Kanyabayonga, baadhi ya watu waliokimbia makazi yao wanajikuta wakilazimishwa kuomba na kufanya kazi katika mashamba ya kibinafsi.

Norbert Sivanzire, mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndani lisilo la kiserikali la Solidarity Action kwa vijana na mazingira endelevu, anaeleza kwa nini:

"Kwa sababu waliokimbia makazi yao hawapati misaada ya kibinadamu mara kwa mara. Kwa mwaka mzima, kulikuwa na mashirika matatu tu ambayo yalijaribu kusaidia waliohamishwa.”

Hadi sasa, maelfu ya kaya zilizohamishwa wanaishi na familia zinazowapokea katika wilaya ya mashambani ya Kanyabayonga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live