Karibia watu kumi wamethibitsihwa kuawaua mjini Goma Mashariki ya DRC, baada ya maofisa wa usalama kujaribu kuzuia maandamano yaliokuwa yamepangwa kufanyika dhidi ya Umoja wa Mataifa kwenye taifa hilo.
Kwa mujibu wa Moleka Maregane, mwanachama wa kundi ambalo lilipanga maandamano hayo, wanajeshi wa DRC waliwaua watu sita katika kituo cha redio na kwenye eneo la ibaada.
Maofisa wa hosipitali kwa upande wao wamesema watu 33 wamelazwa wakiwa na majeraha ambapo wengine watatu wamefariki.
Walioshuhudia tukio hilo na akiwemo meya wa Goma, afisa mmoja wa polisi aliteketezwa wakati wa machafuko hayo.
Walinda usalama wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, wamekuwa kwenye taifa hilo tangu mwaka wa 1999.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukituhumiwa na raia nchini DRC kwa kushindwa kuyakabili makundi ya waasi ambayo kwa muda sasa yamekuwa yakiwahangaisha raia.
MONUSCO inakaribia wanajeshi elfu kumi na sita nchini DRC haswa katika eneo la mashariki.