Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Washerekea kuikomboa Kivu kutoka kwa M23

Vikosi Vya Afrika Mashariki Kusalia DRC Licha Ya Maandamano DRC: Washerekea kuikomboa Kivu kutoka kwa M23

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waandishi wa habari kumi na wawili wameweza kutembelea mji wa kimkakati wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliokombolwa na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Kinshasa, kwa mwaliko wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hivi karibuni kulikuwa na vita vikali baina ya waasi wa M23 ambao serikali ya Kinshasa inalalamika kuwa wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda na wanamgambo watiifu kwa serikali ya Kongo katika eneo la karibu na mji Kitshanga, vita ambavyo vimevunja makubaliano ya amani yaliyodumu kwa miezi kadhaa baina ya waasi hao na serikali ya DRC.

Wanamgambo watiifu kwa serikali ya Kongo wamekomboa mji wa Kitshanga wa Kivu Kaskazini mwezi huu kutoka kwa waasi wa M23 ambao Kinshasa inaishutumu serikali ya Rwanda kuwa inawaunga mkono kwa hali na mali.

Kimsingi na kirasmi ni kwamba jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaheshimu makubaliano ya kusitisha vita na waasi wa M23 lakini makundi ya wanamgambo ambao inadaiwa wanaungwa mkono na serikali, wanaendesha vita dhidi ya waasi hao. Mji wa Kitshanga huko Kivu Kaskazini umeripotiwa kuwa shwari

Hadi wakati inaripotiwa habari hii, mji wa Kitshanga ulikuwa shwari huku wanawake wakiendelea kuuza vyakula sokoni, maduka yalikuwa wazi, na makumi ya watu wenye silaha yaani askari na wanamgambo wanaonekana wakitembea huku na huko katika mji huo.

Mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la John Ishara amenukuliwa akisema: “Kwa sasa tunamshukuru Mungu kwa sababu bado tunaona mchana na tunaona pia Serikali imefika katika mji huu, jambo ambalo ni ishara nzuri ya usalama kuimarika katika mji wetu."

Amesema: "Tunaiomba serikali imfukuze adui na kumlazimika arudi Rwanda, ni wakati huo ndipo tutahisi kuwa salama kabisa."

Mkazi mwingine, Sebunane Rugubaka, yeye amesema, jamii za makabila yote zilikuwa zinaishi pamoja kwa amani lakini inasikitisha kwamba "vita hivi kutoka nchi jirani ya Rwanda vimezusha ubaguzi na kutugawa."

Waasi wa M23 wanaoongozwa na Watutsi walifanya mashambulizi mwishoni mwa 2021 na kuteka maeneo ya Kivu Kaskazini na kusababisha zaidi ya watu milioni moja kukimbia makazi yao.

Eneo la mashariki mwa DRC limekumbwa kwa takriban miaka 30 sasa kutoka kwa makundi yenye silaha ya ndani na nje ya nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live