Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Wapiga kura wagawanyika mwanzoni mwa kampeni

Kuraaa.png DRC: Wapiga kura wagawanyika mwanzoni mwa kampeni

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampeni za uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 20, uchaguzi wa urais, wa wabunge na wa magavana zinaanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumapili Novemba 19. Wagombea 26 wanawania kwenye kiti cha urais , yaani, misafara mingi ya kampeni ambayo itaanza kote nchini. Lengo: kuwashawishi wapiga kura milioni 44.

"Kwa hakika, tunajua kwamba mambo yanaanza siku ya Jumapili": Watu wengi huzungumza kuhusu kampeni ya uchaguzi. Nafasi ya kuchagua kati ya wagombea 26.

“Tunasubiri kila mgombea aweze kuwasilisha sera zake za kampeni na mradi wake wa utawala, na tutaona, tutathmini kile ambacho kila mmoja amezungmzia, tutaamua tumchague nani", amesema édric , mmoja wa wakaazi wa mji wa Kinshasa aliye hojiwa na mwanahabari wetu.

Mbele kidogo, Peter anafanya kazi kwa bidii: yeye ni moja wa wasimamizi wa kampuni ya basi na anasema ana shauku kubwa uchaguzi unapokaribia. “Inatusaidia kwa sababu inasogeza nchi mbele, inaonyesha kuwa nchi ina demokrasia, nchi itasonga mbele na kila kitu kitakuwa bora. Ninajiamini sana kwa hilo. "

Alice, ambaye ni mwanafunzi, anasema atafuata kampeni, lakini zaidi ya yote anataka kura ya uwazi: “kuwa macho sana, hasa katika uchaguzi. Nasisitiza kwa wenzangu kuwa hivyo kwa sababu hatuwezi kuchagua watu, viongozi watakaokuja lakini ambao kwa kweli hawatakuja tu kuongoza. Maana viongozi wakija kwa utapeli ni hatari sana kwetu. Wanakuja kwa maslahi yao wenyewe. Lakini viongozi wanapopata kura zao kwa haki, ni tofauti.

Wakati huo huo, ingawa kila mtu anasema yuko na kadi yake ya kupiga kura, bado hawana uhakika kwamba watapiga kura mnamo Desemba 20.

Wagombea urais wanatarajia kumwaga sera zao kwa wapiga kura katika maeneo mbalimbali ya nchi. Rais Félix Tshisekedi ameamua kuanza katika mji mkuu wa Kinshasa kwa mkutano mkubwa Jumapili Novemba 19 huko Stade des Martyrs. Wapinzani wake wakuu watakuwa katika mikoa: Moïse Katumbi anatarajiwa Kisangani, Martin Fayulu atakuwa Bandundu wikendi hii katika ngome yake.

Haiwezekani kuorodhesha programu ya kampeni ya wagombea 26, lakini wengi wao wataenda kwanza mashariki mwa nchi, katika eneo linalokumbwa na migogoro. Hii hasa katika mpoa wa Kivu Kaskazini ambako maeneo ya Rutshuru na Masisi hayataweza kupiga kura kutokana na kuwepo kwa uasi wa M23.

Sio tu wagombea urais ambao watafanya kampeni: wagombea kwenye viti vya ubunge na kwenye nafasi za magavana wanaanza kampeni zao leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live