Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Wanaokimbia makazi yao wanaelekea Goma kwa wingi...

GOMA DRC.png DRC: Wanaokimbia makazi yao wanaelekea Goma kwa wingi...

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nje kidogo ya Goma, moja ya miji mikubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kambi za watu waliokimbia makazi yao zimejaa tangu karibu kuanza kwa vita dhidi ya waasi wa M23. Wakazi wanakabiliwa na uhaba wa maji, umeme, chakula na hawana makazi.

Na tangu mapigano yaanze tena mwanzoni mwa mwezi Oktoba kati ya M23 na jeshi la Kongo linaloshirikiana na makundi yanayoiunga mkono serikali, watu waliokimbia makazi yao wamekuwa wakiwasili karibu na Goma kila siku.

Olivier ni mwalimu. Takriban mwezi mmoja uliopita alitoroka kijiji chake kwa kukimbia mapigano. Anatuonyesha sehemu anakolala: "Mimi kiongozi". "Nyumba yake iliyozunguushwa kwa miti huku ikizunguukwa na vibanda vidogo vilivyojengwa kwa miti na udongo.

Mvua imetoka tu kunyesha, watoto wawili wanadondoka kwenye dimbwi kubwa la maji yenye matope: "Ili kupata maji hapa, unahitaji pesa. Hawana pesa, hawana chochote. Kwa hiyo watoto wanachukua maji hayana kuosha nyuso zao. Na hiyo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa. » Hali ya kutisha

Hali mbaya sana ambazo Olivier anakabiliana nazo. Mamlaka ya Kongo au wahusika wa masuala ya kibinadamu hawaingilii kati ili kusaidi au kuhudumia kambi hii mpya iliyofunguliwa katikati ya mwezi wa Oktoba na ambayo tayari ina angalau watu 6,000: "Hiyo ndiyo ofisi ya kambi mpya". Innocent Tumaini ndiye mkuu wa kambi hii mpya, inayoitwa Cepac. Sio mara ya kwanza kwa mapigano kuathiri kijiji chake cha asili lakini ni mara ya kwanza kuamua kukihama. "Ni kifo"

Sababu? Kuibuka kwa makundi yanayounga mkono serikali, yanayoitwa Wazalendo: “Naogopa kukaa huko. Kwa nini? Kwa sababu hakuna usalama wowote. Ukienda shambani kuna Wazalendo utakutana nao. Na Wazalendo wanapokutana na M23, kunatokea makabiliano makubwa, na hapo ndipo unakiona kifo mbele yako. Ili kuepuka hili, tunaona ni bora kuwa katika maeneo haya mekundu. Wakimbizi wapya wanatarajiwa katika kambi hizo. Kwenye uwanja wa vita mapigano yanapamba moto katika maeneo kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live