Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Wanakijiji wachinja tembo na kumla nyama

Utafiti Kinyesi Cha Tembo Kenya Unaonyesha Wanakula Lishe Tofauti DRC: Wanakijiji wachinja tembo na kumla nyama

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANAKIJIJI wa Katwiguru, Kivu Kaskazini karibu na Mbuga ya Taifa ya Virunga iliyopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamechinja na kula nyama ya tembo aliyetoroka kutoka mbugani.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), tembo huyo alichinjwa na wakazi hao walionukuliwa na kundi la wahifadhi la Conserv Congo wakisema walikuwa na furaha kwani hiyo ilikuwa kama neema iliyowashukia kutoka mbinguni.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Taasisi ya Kuhifadhi Mazingira ya DRC (ICCN) ilisema haijabainika iwapo tembo huyo aliuawa na waasi au wanakijiji hao.

Shirika la habari la AFP pia liliripoti kuwa ICCN ilisema awali, tembo wawili walikuwa wakitangatanga nje ya mbuga ya wanyama baada ya vijana kuharibu kizuizi cha umeme kilichowekwa kuzunguka eneo hilo hivi karibuni.

Haijafahamika nini kilitokea kwa tembo wa pili.

Mbuga hiyo pia ipo kwenye mpaka na Rwanda na Uganda. Tovuti ya mbuga hiyo inasema mamalia wake mashuhuri zaidi ni pamoja na tembo wa msitu na savanna, viboko, simba na sokwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live