Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Wanajeshi wa serikali wadhibiti hali katika mji wa Masisi

DRC DRC MASISI.png DRC: Wanajeshi wa serikali wadhibiti hali katika mji wa Masisi

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya utulivu imeshuhudiwa jana Alhamisi Februari 15, 2024, kwenye karibu ngome zote za mapigano katika eneo la Masisi -Kivu Kaskazini.

FARDC, inayoungwa mkono na vijana wazalendo, ambao wameendelea kudhibiti ngome zao huko Sake na Bweremana karibu na Shasha mji unaokaliwa na waasi wa M23/RDF tangu juma lililopita.

Kukaliwa kwa mji wa Shasha na kundi la M23/RDF kumesababishwa kusitishwa kwa shughuli za usafiri kati ya Sake na Minova barabara pekee iliokuwa imesalia kusambaza chakula na bidhaa nyingine kwenda Goma.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mashirika ya kiraia huko Masisi, Voltaire Batundi, hali bado haitabiriki, baada ya mapigano hayo kuripotiwa siku ya Jumatano, kwenye milima inavyoutazama mji wa Shasha.

Wakati huo huo, idadi ya watu waliokimbia makazi yao imeendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali huko huko Goma, haswa huko Bulengo, iliyoko katika wilaya ya Lac Vert, magharibi mwa jiji.

Watu hawa waliolazimishwa kukimbia wanatoka hasa Shasha, Sake na maeneo ya jirani.

Wanakimbia mapigano mapya, ambayo yamezuka hivi karibuni kati ya FARDC, inayoungwa mkono na Wazalendo, na waasi wa 23/ wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda

Chanzo: www.tanzaniaweb.live