Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Wagombea watoa wito kufutwa matokeo Uchaguzi Mkuu

Tume Ya Uchaguzi DRC Yafuta Uchaguzi Katika Majimbo Kadhaa DRC: Wagombea watoa wito kufutwa matokeo Uchaguzi Mkuu

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wagombea wanane wa urais na viongozi wengine wa kisiasa nchini DRC wametoa wito wa kufutwa kwa uchaguzi wa pamoja wa Desemba 20, 2023, wanaodai uligubikwa na udanganyifu.

Wakizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa juma lililopita, waliokuwa wagombea, Anzuluni, Diongo, Fayulu, Katumbi, Kikuni, Matata, Mukwege na Sesanga wamesema hatua ya CENI kufuta baadhi ya matokeo, kunathibitisha madai yao.

Katika taarifa yao wamesema "Uchambuzi rahisi wa orodha ya wagombea wa nafasi mbalimbali 82 unaonyesha kuwa udanganyifu ulifanyika katika maeneo mengi ya nchi na kwamba hali ni mbaya kulingana na ushahidi uliowekwa wazi hadi sasa.

Aidha walionesha kushangazwa na tume ya uchaguzi, kukiri kuwa uchaguzi wa wabunge ndio uliokuwa na dosari pekee na sio uchaguzi wa urais wakati uliunganishwa katika karatasi moja ya kura.

Wagombea hao wanaituhumu tume ya uchaguzi kuwatumia wakuu wa uchaguzi wanaodai wana uhusiano na familia ya rais Felix Tshisekedi, tuhuma ambazo CENI imeendelea kukanusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live