Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Wabunge wa Nord-Ubangi 'wamtimua' Gavana mjukuu wa Mobutu

DRC: Wabunge Wa Nord Ubangi 'wamtimua' Gavana Mjukuu Wa Mobutu DRC: Wabunge wa Nord-Ubangi 'wamtimua' Gavana mjukuu wa Mobutu

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Wabunge katika jimbo la Nord-Ubangi kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepiga kura ya kumtimua Gavana Malo Ndimba Mobutu wa jimbo hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Malo Mobutu, 41, ni mjukuu wa Maréchal Mobutu Sese Seko ambaye alitawala Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) kwa miaka 32 hadi 1997, alipopinduliwa na waasi wakiongozwa na Laurent-Désiré Kabila.

Vyombo vya habari vya DRC, ikiwa ni pamoja na Radio Okapi ya Umoja wa Mataifa, vinaripoti kuwa Malo Mobutu alitimuliwa katika kura ya kutokuwa na imani iliyofanyika Jkatika Bunge la Jimbo la Nord-Ubangi Jumamosi.

Vyombo vya habari vya RTNC vya Congo viliripoti kwamba Malo Mobutu alipigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge wengi 10 kati ya wabunge 18 wa bunge la mkoa.

Habari zinasema kuwa wabunge hao walimshutumu kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa fedha nukiwemo ubadhirifu wa baadhi ya fedha zilizokusudiwa kwa ajili ya kazi za umma katika jimbo hilo.

Malo Mobutu hajatangaza hadharani chochote kuhusu uamuzi huo na mashtaka dhidi yake. Inasemekana hakuwapo bungeni wakati kura dhidi yake ilipopigwa

Chanzo: Bbc