Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Video ya waziri kuhusu adhabu dhidi ya wapenzi wa jinsi moja yazua gumzo

Video Ya Waziri Mkuu DRC: Video ya waziri kuhusu adhabu dhidi ya wapenzi wa jinsi moja yazua gumzo

Thu, 30 May 2024 Chanzo: Bbc

Video kuhusu adhabu dhidi ya wapenzi wa jinsi moja iliyotoleawa na waziri mpya wa sheria aliyeteuliwa wiki hii imeibua gumzo nchini DRC hususan miongoni mwa watumiaji wa mitandao yakijamii nchini humo.

Katika video hiyo Waziri Constant Mutamba anaonekana akiahidikuidhinisha kifungo cha kati ya miaka mitano hadi kumi na tano na faini ya pesa milioni 30 franga za Congo. Takriban dola za Kimarekani 10,000.

"Mapenzi kati ya baba na baba, mama na mama, utafungwa miaka tano hadi kumi na tano jela, mambo haya yanapaswa kumalizika, utalipa faini ya milioni 30 pesa za Congo," anasema Constant Mutamba katika video hiyo iliosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na BBC, waziri huyu wa sheria, amesema, video hii ilirekodiwa mwezi moja kabla uteuzi wake kama waziri, na ni mswada wa sheria ambao aliwasilisha bungeni baada ya kuchaguliwa kama mbuge na kuteuliwa kuwa waziri nah atua hiyo haitamzuia kuendeelea na mswada huo.

''Video hiyo kweli ni yangu ilirekodiwa mwezi moja kabla kuteuliwa kwangu, lakini nimewahakikishia ya kwamba hiyo ni moja ya vipaumbele vyangu, ni moja ya mswada wangu wa sheria'' na nitaendelea kufuatilia, mapenzi ya jinsia moja hayawezi kamwe kukubaliwa Katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo’’ amesisitiza Constant Mutamba Tungulu, ambae ni waziri mpya wa sheria.

Je sheria ya DRC inasema nini kuhusu wapenzi wa jinsia moja?

Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi Congo, sheria rasmi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja haipo,lakini mila na utamaduni wa nchi hizo vinapinga kabisa mapenzi ya aina hiyo, na kutajwa kuwa ni kinyume na mila.

Kulingana kipengele cha 40 cha Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo "kila mtu ana haki ya kumuoa mtu anayemtaka, wa jinsia tofauti na kuanzisha familia, yaani ndoainayofungwa kati ya mume na mke pekee.

Siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema msimamo wa Washington kuhusu suala hilo "utabadilika na kurekebishwa" kulingana na mabadiliko ya hali ilivyo vitani. Kwa sasa yuko katika mji mkuu wa Czech, Prague, kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Nato.

Msemaji wa usalama wa taifa wa White House John Kirby alisema jioni Jumatano kwamba ingawa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine umebadilika, "hivi sasa, pia hakuna mabadiliko katika sera yetu".

Ukraine imekuwa ikijitahidi kukabiliana na mashambulizi ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo, huku jiji la Kharkiv likikumbwa na mashambulizi mabaya ya wiki kadhaa, ambayo mara nyingi huanzishwa na Urusi kutoka kwa vituo vya kijeshi karibu na mpaka wa Ukraine.

Kauli ya Bw Blinken, wakati wa safari yake barani Ulaya, ilifuatia maoni ya moja kwa moja zaidi yaliyotolewa mapema wiki hii na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alisema Ukraine inapaswa "kuruhusiwa" kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi dhidi ya maeneo ya kijeshi katika ardhi ya Urusi - ingawa hailengi raia kabisa.

Chanzo: Bbc