Huko Tshopo, nchini DRC, mzozo wa ardhi ambao uligeuka kuwa mzozo wa kikabila umeanza tena baada ya utulivu mwishoni mwa mwaka. Mgogoro huu tayari umesababisha zaidi ya vifo 500 tangu mwezi wa Februari 2023. MSF inaonya juu ya hali ya kibinadamu.
Mvutano kati ya jamii mbili, Mbolé na Lenga ulikuwa umepungua mwishoni mwa mwaka 2023, lakini tangu mwanzoni mwa mwezi wa Januari 2024, mapigano yazuka tena, na kusababisha watu wengi kutoroka makazi yao.
Hali ambayo inatia wasiwasi shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka, ambalo limepeleka tume wafanyakazi wake, anaelezea Alira Halidou, mkuu wa ujumbe wa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka nchini DRC, akihojiwa na Paulina Zidi wa chumba cha habari cha RFI kitengo cha Afrika.
"Baada ya takriban miezi miwili ya utulivu, uhasama ulizuka tena tangu mwez wa Januari 2024. Vibanda vimechomwa moto na kumerekodiwa waathiriwa wengine na watu kadhaa kujeruhiwa.