Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC : Tshisekedi na Katumbi wanavyochuana kwenye Urais

Tshisekedi Katumbi Urais.png DRC : Tshisekedi na Katumbi wanavyochuana kwenye Urais

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa DRC Félix Tshisekedi na mpinzani wake Moïse Katumbi ndio wagombea ambao wameorodheshwa katika nafasi ya juu katika uchaguzi ambao umepangwa kufanyika mwezi ujao huku wawili hao wakiwa wameimarisha kampeni zao kwa kuzuru zaidi ya mikoa mitano kuelekea uchaguzi wa Disemba 20.

Wiki moja tu baada ya kampeni rasmi kuanza nchini DRC, vitengo vitano vya wagombea mbalimbali vimechipuka kuhusiana na jinsi ambavyo wanaendesha kampeni zao.

Wagombea wawili, rais Félix Tshisekedi and Moise Katumbi, wamejitambulisha kwa raia kwa mtindo wa kutumia rasilimali muhimu kufanya kampeni.

Rais Tshisekedi ambaye anawania urais kwa muhula wa pili tayari amefanya kampeni zake katika mikoa ya Kinshasa alipozindua kampeni yake, Kongo-Central, Maniema, Équateur na Ubangi Kaskazini.

Aidha mpinzani wake Katumbi ambaye kampeni yake inaangazia kurejesha amani, uboreshaji wa kijamii na ujenzi wa kitaifa amefanya kampeni katika mikoa sita ya Tshopo, Kivu Kusini, Haut na Bas-Uele, Ituri na North Kivu.

Kando wawili hao, kundi lingine ni lile la Martin Fayulu, Denis Mukwege, na Delly Sesanga ambalo pia linafanya kampeni kivyao.

Tayari Matata Ponyo, Seth Kikuni na Franck Diongo walijiondoa na kumuunga mkono Moïse Katumbi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live