Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Tshisekedi ataka MONUSCO kuondolewa haraka

Tshisekedi Aonya Mtafaruku Wa Maaskofu DRC: Rais Tshisekedi anataka mpango wa kuondoa MONUSCO kuharakishwa

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi akitoa hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametaka kuharakishwa kwa mchakato wa kukiondoa nchini mwake kikosi cha kulinda amani MONUSCO ambacho kimekuwa nchini hiyo kwa miaka zaidi ya 20.

Tshisekedi amesema wakati umefika wa DRC kuchukua udhibiti wa nchi yake, huku akikishtumu kikosi hicho kwa kushindwa kumaliza utovu wa usalama, Mashariki mwa nchi yake.

Kiongozi huyo amesema ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umekosa kurejesha amani mashariki ya taifa lake licha ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 25.

“Sio haki na haikubaliki watu wanaotajawa kuhusika na uhalifu mkubwa uliotajwa katika ripoti mbalimbali za wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya usalama nchini DRC wamesalia bila kuadhibiwa.” alisema rais Tshisekedi.

Monusco ina wanajeshi zaidi ya elfu kumi na sita nchini DRC na ni ya pili katika ukubwa duniani.

Walinda amani hao wamekuwa wakituhumiwa hata na raia wa taifa hilo kwa kile wanachodai ni kufeli katika majukumu yao, baadhi ya raia wakionekana kuaandamana wakiwataka waondoke kwenye taifa hilo.

Makundi ya waasi yameendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya raia katika baadhi ya maeneo ya mashariki ya DRC hali ambayo imepelekea kutumwa kwa wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusaidia katika urejeshwaji wa amani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live