Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Takriban watu 24 wafa maji baada ya boti ya kupinduka

DRC: Takriban Watu 24 Wafa Maji Baada Ya Boti Ya Kupinduka.png DRC: Takriban watu 24 wafa maji baada ya boti ya kupinduka

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Takriban watu 24 wamefariki katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya mashua iliyokuwa imejaza mizigo kupinduka kwenye mto katika jimbo la Mai-Ndombe nchini Kongo, na idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka huku abiria wengi wakitoweka, afisa mmoja wa eneo hilo alisema Jumatano.

Boti iliyobeba takriban abiria 250 hadi 300 ilipinduka Jumapili usiku baada ya kugonga vizingiti chini ya maji, msimamizi wa eneo la Kutu Jacques Nzenza aliliambia shirika la habarila Reuters.

Kupakia watu na miziko kupita kiasi ndio chanzo kikuu cha ajali hiyo, alisema. "Kulikuwa na wasi wasi katika boti na watu waliojawa na hofu walienda kwenye sehemu moja kuweka uzito upande mmoja, na kusababisha mashua kupinduka."

Kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo, Fidele Lizoringo, amesema watu 43 walinusurika lakini wanakijiji waliokuwa na hasira walimpiga meneja wa boti hiyo kwa sababu baadhi ya ndugu zao walikufa katika ajali hiyo.

Usafiri wa kwenye mito na ajali mbaya za boti ni jambo la kawaida katika nchi hiyo ya Afrika ya kati, ambayo ina barabara chache za lami katika eneo lake kubwa lenye misitu na vyombo vya usafiri mara nyingi hupakiwa kupita uwezo wake.

Chanzo: Bbc