Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Shule ya ubalozi wa Ubelgiji jijini Kinshasa yafungwa

Vikosi Munucos DRC DRC: Shule ya ubalozi wa Ubelgiji jijini Kinshasa yafungwa

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lycee Prince de Liege ilio chini ya ubalozi wa Ubelgiji jijini Kinshasa imefunga milango yake kuanzia leo Jumatatu, kufuatia hofu ya kutokea kwa machafuko, huku balozi kadhaa za magharibi na mashirika ya kimataifa yakiwataka watu wake kutotumia magari yao ya kazi katika barabara za jiji la Kinshasa.

Hofu hii imekuja baada ya kushudiwa vurugu jumamosi iliopita jijini Kinshasa ambapo magari kadhaa ya shirika la Umoja wa Mataifa Monusco yakiteketezwa moto, ambapo Umoja wa Mataifa umewataka wafanyakazi wake jijini Kinshasa kuwa makini.

Haya yanajiri wakati huu wito ukitolewa kwa serikali ya Kinshasa kuanzisha uchunguzi kubaini wahusika na kuwaadhibu kwa mujbu wa sharia.

Maandamano yalizuka mjini Kinshasa, yakilenga wawakilishi wa kidiplomasia na mashirika ya kimataifa, Jumamosi Februari 10. Vijana waliokuwa na hasira walichoma matairi katika baadhi ya ya jijini Kinshasa.

Kiongozi mmoja wa upinzani amelaani matukio hayo na kuwashutumu vijana wa chama tawala kuhusika na vurugu hizo, utawala ambao unataka kuwanyamanzisha wanadiplmasia ambao wamekuwa wakikosoa, huku mwingine akidai kuwa huwezi kuwavika wananchi matukio hayo.

Kwa upande wake, serikali ya DRC imelaani vikali vitendo hivi vya vurugu na kuzidisha ulinzi katika ofisi za kidiplomasia na Monusco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live