Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Shirika la misaada laonya hali mbaya ya kibinadamu Ituri

Wakimbizi Ituri Drc.png DRC: Shirika la misaada laonya hali mbaya ya kibinadamu Ituri

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kutoa misada kwa wakimbizi kutoka Norway (NRC) linapaza sauti juu hali ya wasiwasi katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mkoa wa Ituri unakabiliwa na ghasia kutoka kwa vmakundi yenye silaha, haswa waasi kutoka Uganda wa Allied Democratic Forces (ADF) na wanamgambo wenye silaha wa Codeco.

Zaidi ya watu milioni 1.6 kwa sasa wameyahama makazi yao huko Ituri. "Jumuiya ya kimataifa inapaswa kusitisha tabia ya kutojali raia wa Ituri na kuchukua hatua za haraka kuwasaidia kuweka misingi ya mustakabali wa amani," inahimiza NRC.

Akihojiwa na RFI, Eric Batonon, mkurugenzi wa shirika la NRC nchini DRC, anaishi mjini Goma, ana wasiwasi kuhusu ugumu wa kufadhili misaada ya kibinadamu nchini DRC, ugumu, ambao anasema, unaoongezeka kuhusu Ituri, mgogoro uliosahaulika. "Mgogoro unaoongezeka"

"Ni wazi, hali ya kibinadamu imekithiri huko Ituri," amesema. Hata hivyo, kama tunavyojua vyema, tatizo la kufadhili dharura za kibinadamu bado ni tatizo kubwa na kama tunavyojua pia, kuna migogoro kila mahali duniani ambayo mara nyingi inamaanisha kuwa mgogoro wa DRC umesahaulika. Ni kweli pia kwamba umakini uliongezwa kwa mkoa wa Kivu Kaskazini na, mzozo huu wa kundi la waasi la M23 kwa bahati mbaya umesababisha kupuuza, kidogo, kwa hali ya Ituri. " "Mshikamano"

"Kwa sasa, kuna haja ya kweli, si tu katika ngazi ya dharura, lakini pia haja ya kuanza kufanya kazi ya kubadilisha mgogoro, juu ya uwiano wa kijamii na kuruhusu kwamba, hatua kwa hatua, pale ambapo tunaweza, wilaya kwa wilaya, kijiji kwa kijiji, eneo kwa wilaya, kuweza kuleta mshikamano, kuweza kuleta amani. Kubadilisha mzozo, kwa sasa, ni jambo ambalo lazima pia tuwekeze ili kuwa na uhakika kwamba tunafanyia kazi sababu za mzozo huo,” anahitimisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live