Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Serikali yatakiwa kuzuia mauaji ya wanawake Lubumbashi

DRC: Jeshi Larejesha Utulivu Katika Mji Mdogo Wa Sake Uliodhibitiwa Na M23 DRC: Serikali yatakiwa kuzuia mauaji ya wanawake mjini Lubumbashi

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watetezi wa haki za binadamu kwenye mji wa Lubumbashi nchini DRC, wametoa wito kwa serikali kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, baada ya tukio la mwishoni mwa juma lililopita, ambapo mwanamke mmoja aliuawa kikatili na mumewe kwenye mji wa Kasumbalesa.

Picha kwenye mitandao ya kijamii imemuonyesha mwanamke husika akiwa amefungwa kamba, mwili wake pia ukionekana kuwa na majeraha makubwa.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, mauaji hayo yalitokea baada ya mabishano kati ya wawili hao.

Mauaji haya yametokea wakati huu mashirika ya kiraia yakiendelea na kampeni kuhusu kuheshimiwa kwa haki za wanawake. Dorcas Kazadi, ni kiongozi wa shirika Rien Sans la femme.

''Hatutaki tena kuendelea kuripotiwa kwa matukio kama haya ambapo wanawake wanauawa na waume wao.’’ alisema Dorcas Kazadi, kiongozi wa shirika Rien Sans la femme.

Mhusika wa mauaji haya alidaiwa kutoroka baada ya kuhifadhi mwili wa marehemu katika chumba cha kuhifadhi maiti. Didier Kapend, mkuu wa Shirika Doctors Human Rescue anataka mhusika kuwajibishwa.

“ Tunatoa wito kwa serikali kumkamata mhusika na kufikishwa mahakamani.’’ alieleza Didier Kapend, mkuu wa Shirika Doctors Human Rescue.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live