Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Serikali kutatua msongamano gereza la Makala

Gerezani Makala Drc.png DRC: Serikali kutatua msongamano gereza la Makala

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini DRC, mamlaka ilimtuma hakimu mkuu katika gereza la Makala Jumatatu Machi 25 kuangalia tatizo la msongamano wa wafungwa. Ombi ambalo linakuja baada ya kuachiliwa kwa mwanahabari Stanis Bujakera, ambaye alielezea tatizo hili katika gereza kuu la Kinshasa. Taarifa kutoka kwa mwanahabari huyo ilizua taharuki hadi serikalini na kuangazia hali ya kipekee ya mfungwa mmoja , ambaye anazuiliwa kwa miaka 21.

Akiwa anashukiwa kwa "wizi wa kutumia silaha", Damas Ngoy Kumbu alikamatwa Oktoba 3, 2003: askari huyu mwenye umri wa miaka 56 kwa hiyo anazuiliwa kwa miaka 21. Habari zilizothibitishwa na mwanasheria wake mpya, Wakili Atweka Pamba ambaye amekuwa akimtetea mteja huyu tangu mwaka 2020. Bila maendeleo madhubuti licha ya kusikilizwa kwa kesi, wakili huyo sasa anategemea kuhusika kwa Hakimu kiongozi wa Mahakama ya Juu.

Siku ya Jumatatu Machi 25, Hakimu kiongozi wa Mahakama ya Juu Elie Ndomba Kabeya alitembelea gereza la Makala kukutana na Damascus Ngoy Kumbu. Baada ya kuwasili, Hkimu kiongozi alisema: “Gereza hili limekuwa chafu kabisa, nimetahadharishwa. Kuzungumza ni vizuri, lakini lazima tuangalie. Sisi ni mawakili na nitafuatilia faili hili.” Kulingana na habari zetu, watu hao wawili walionana lakini hakuna kilichovuja kwenye mkutano huu.

Ziara hii katika gereza kuu ni matokeo ya ombi la moja kwa moja kutoka kwa Mkuu wa Nchi. Wakati wa kikao cha baraza la mawaziri siku ya Ijumaa Machi 22, Félix Tshisekedi aliwataka mawaziri wake, haswa waziri wa Sheria, kumpa ndani ya siku nane habari zote kuhusu hali ilivyo katika magereza, Huku akikumbusha hasa kwamba "haki ya kuhukumiwa kwa wakati ufaao ni haki ya kikatiba".

Kabla ya hapo, Rais Félix Tshisekedi mnamo Februari 22, kwenye RFI, alibaini kwamba "atajihusisha" kwenye faili ya mwanahabari Stanis Bujakera. Hii bila kutarajia kwamba mwandishi huyu wa habari, baada ya kuachiliwa, alizungumzia kuhusu hali ya msongamano wa wafungwa huko Makala, gereza kuu la Kinshasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live