Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Sababu za kucheleweshwa kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi

Uchaguzi DRC 2023: Rais Felix Tshisekedi Atangazwa Kushinda Kwa Kishindo DRC: Sababu za kucheleweshwa kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa kitaifa na mikoa yanasubiriwa kwa hamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tume huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) ilipaswa kutangaza matokeo ya uchaguzi wiki moja iliyopita, Januari 3, lakini ilibidi kuahirisha tarehe hiyo hadi tarehe nyingine itayotangazwa baadaye. Wajumbe 15 wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi wanakutana tangu kufanyika kwa uchaguzi. Kulingana na vyanzo kutoka CENI, ucheleweshaji huu unaelezwa kwa mambo kadhaa.

Hapo awali CENI ilichelewa kwa sababu ya ujumuishaji mrefu wa matokeo. Kwa sababu kwa uchaguzi wa wabunge na madiwani, inataka kuzingatia kadi za kupigia kura. Operesheni hii ilifungwa siku tano zilizopita, kulingana na vyanzo vya ndani, Tum Huru ya Uchaguzi ilichunguza visa vya udanganyifu, ufisadi na ujazo wa kura.

Wagombea themanini na wawili waliona kura zao zimebatilishwa na kura kufutwa katika miji miwili, Yakoma na Masimanimba. Hili ndilo lililochelewesha uchapishaji wa matokeo katika siku za hivi karibuni. Kwa sababu CENI lazima ichunguze visa vingine vilivyoripotiwa vya udanganyifu na uwezekano wa kupanua orodha. Ni lazima pia kuchunguza rufaa za hiari zilizowasilishwa na wengi wa wagombea 82.

Baadhi wamepeleka suala hilo kwa Baraza la Kitaifa, ambalo lilichukua suala hilo mikononi mwake siku ya Jumatano na linatarajiwa kutoa uamuzi wake siku ya Ijumaa.

Hata kama wanasheria wanabaini kwamba rufaa hizi kwa sasa zinajumuisha kizuizi kikubwa cha uchapishaji wa matokeo, maafisa wa Céni bado wanaamini kuwa wanaweza kutangaza matokeo kulingana na eneo. "Wacha tuanzie ambapo hatujagundua ufisadi na matukio yoyote."

Rasmi, sekretarieti ya utendaji ya CENI, chombo cha kiufundi, kiliwasilisha kwa mwenyekiti wake orodha ya vyama vya siasa na makundi yaliyofikia kizingiti cha 1% ya kura zilizopigwa. Vyama vilivyopata 1% pekee ndivyo vitaweza kuketi Bungeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live