Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Rais Tshisekedi amshutumu Joseph Kabila kuunga mkono waasi

DRC: Rais Tshisekedi Amshutumu Joseph Kabila Kuunga Mkono Waasi.png DRC: Rais Tshisekedi amshutumu Joseph Kabila kuunga mkono waasi

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Congo Felix Tshisekedi amemshutumu kiongozi wa zamani Joseph Kabila kwa kuhusika na muunganisho wa kundi la waasi la AFC-M23 linalopigana dhidi ya utawala wake mashariki mwa nchi hiyo.

"Katika mahojiano ya faragha na wanahabari wawili wa Congo, vyombo vya habari vya Congo Independent na Top Congo, Tshisekedi alimshutumu Kabila kwa kuwa nyuma ya AFC.

Alisema Kabila alikataa kushiriki uchaguzi wa mwaka jana na alikuwa akipanga uasi wa AFC.

Akijibu tuhuma hizo, kiongozi wa chama cha Joseph Kabila aliambia BBC kwamba madai haya hayana msingi, na akasema ni bahati mbaya.

Ferdinand Kambere aliongeza kuwa hii inaonyesha kuwa Tshisekedi hana ufahamu wa kina wa hali ya usalama mashariki mwa DR Congo.

AFC-M23 haijatangaza lolote kuhusu madai haya mapya ya Tshiseked dhidi ya rais huyo wa zamani wa DRC.

Bwana Tschisekedi hakutoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake.

Shutuma za Tshisekedi zinafuatia tangazo la Marekani la vikwazo dhidi ya AFC mwezi uliopita.

Washington iliushutumu muungano huo kwa kutaka kuipindua serikali ya DRC na kuchochea mzozo mashariki mwa nchi hiyo.

Ilisema mwanachama mkuu wa muungano huo, kundi maarufu la waasi la M23, tayari liko chini ya vikwazo vya Marekani.

Chanzo: Bbc