Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Raia wa 5 wameuawa katika mashambulio ya mabomu wakati mapigano makali

DRC: Raia Wa 5 Wameuawa Katika Mashambulio Ya Mabomu Wakati Mapigano Makali DRC: Raia wa 5 wameuawa katika mashambulio ya mabomu wakati mapigano makali

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Raia wa 5 wameuawa katika eneo la Nyanzale katika katika mashambulio ya mabomu wakati wa mapigano makali kati ya M23 na wanajeshi wa DRC wilayani Rutchuru.

Haya yanajiri siku chache tuu baada ya Majeshi ya Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na SADC,wakishirikiana na Majeshi ya Congo FARDC pamoja na hayo ya BurundiI kusema kuwa yanaweka mikakati muhimu ya kuimarisha operesheni zao za pamoja kwa lengo la kuleta amani na Usalama mashariki mwa Congo.

Tangu Juma mosi juma lililo pita hadi sasa ni raia 7 ndio wamepoteza maisha baada ya mabomu kurushwa na wale wanaoaminika kuwa waasi wa M23, ambao wamekuwa wakikalia karibu vilima vyote vinavyoutazama mji wa Sake katika eneo la Kivu Kaskazini ,lakini piya Eneo la Nyanzale Wilayani Rutchuru.

Haya yalitokea muda mfupi kabla ya kuwasili kwa wakuu wa vikosi vya ulinzi vya Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Burundi katika eneo la Mubambiro lakini piya Eneo la Nyanzale hapo jana baada ya Majeshi hayo kuondoka jijini Goma.

‘’Hali hii imewaathiri raia wengi ambao wamelazimika kuhama makwao na sasa wanaishi kambini…’’, anasema muwakilishi wa Gavana wa Nyanzale.

‘’Viongozi wa jeshi waliotembelea eneo hili wamesema kuwa wanaweka mikakati tofauti ili kurejesha usalama katika eneo hili.’’, mmoja wa raia waliathiriwa na mapigano ambaye yuko kambini

Huku hayo yakijiri, raia wengi wanasema kuna haja ya juhudi za haraka za kuleta amani ya kudumu katika eneo hili.

Chanzo: Bbc