Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Mshindi wa uchaguzi wa urais kutangazwa Jumapili wiki hii

Uchaguzi DRC: Shughuli Ya Kuhesabu Kura Inaendelea Katika Baadhi Ya Vituo DRC: Mshindi wa uchaguzi wa urais kutangazwa Jumapili wiki hii

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inatarajiwa kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais hapo kesho, baada ya mamilioni ya wananchi kupiga kura wiki iliyopita.

Tangazo hilo, limetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi CENi, Denis Kadima, ambaye amesema tume hiyo itaheshimu muda wa matokeo hayo kutolewa.

Kufikia siku ya Ijumaa, CENI inasema ilikuwa imehesabu kura karibu Milioni 16, huku matokeo yakionesha kuwa rais Felix Tshisekedi anayetaka kuwania kwa muhula wa pili, akionekana kuongoza dhidi ya wapinzani wake.

Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 20, umekosolewa na wagombea wa upinzani ambao siku ya Jumatano, waliandaa maandamano jijini Kinshasa, kushinikiza kufutwa kwa uchaguzi huo.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa, yanatarajiwa kuthibitihswa na Mahakama ya Katiba mwezi Januari, huku mshindi akitarajiwa kuapishwa Januari 20.

Waangalizi wa ndani kutoka mashirika ya kiraia na wale wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, CENCO wamekosoa namna uchaguzi huo ulivyofanyika na kusema dosari nyingi zimeshuhudiwa.

Wananchi wa DRC walipiga kura Desemba 20 lakini zoezi hilo likaendelea kwa siku kadhaa katika baadhi ya maeneo ambayo hayakupokea vifaa vya kupigia kura kwa wakati, zoezi ambalo limekosolewa ni kinyume cha utaratibu wa Tume ya Uchaguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live