Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC : Masuala ambayo raia watazingatia kabla ya kumchagua rais mpya

Tshisekedi Aonya Mtafaruku Wa Maaskofu DRC : Masuala ambayo raia watazingatia kabla ya kumchagua rais mpya

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati huu raia wa DRC wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwezi ujao na wagombea wa nafasi mbalimbali kuendelea kunadi sera zao, utendakazi unatarajiwa kuwa kipimo kwa rais Felix Tshisekedi, anayetaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Baadhi ya maswala ambayo yatazingatiwa na wapiga kura, ni pamoja na hali ya kiuchumi nchini humo ambapo licha ya nchi hiyo kuwa na raslimali za kutosha ikiwemo madini, kiwango cha umaskini kiko kwenye asilimia 62 kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2020 ya shirika la Notre Dame Global Adaptation Index.

Aidha, kupanda kwa gharama ya maisha na kushuka kwa thamani ya Faranga ya Kongo ni jambo lingine ambalo raia watazingatia wakati wa kupiga kura.

Usalama, haswa mashariki mwa nchi ambako makundi ya waasi kama vile ADF, CODECO na M23 yameendelea kuwahangaisha raia ni jambo nyeti linalogusa raia wakati huu wakiwa hawajaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti usalama.

Kadhalika, suala la rushwa, pia linatazamwa ambapo wakosoaji wanaona ni tatizo lililokuwa sugu katika taasisi za uma nchini humo, moja ya sera ambayo inatumika na wapinzani wa Thsisekedi kuonesha ameshindwa kazi.

Suala la mwisho ni ikiwa tume ya uchaguzi nchini humo pamoja na Serikali, zitaweza kuandaa uchaguzi ulio huru, haki na kuaminika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live